Kwenye wadi wa kuamka


Baada ya upasuaji, mtoto huhamishwa kwenye wadi/chumba cha kuamka.

Daktari (surgeon), aliyempasua kwa kawaida atakuja kuwapa wazazi/walezi habari za matokeo.

Kwa hiyo ni bora ukipatikana katika chumba cha kusubiri ambapo tayari upasuaji.

Umsubiri mwuguzi atakayekuita na kukusindikiza hadi chumba cha kuamka.

Wadi ya kuamka,ni chumba kikubwa chenye nafasi kwa watoto wengi wa umri tufauti.

Kuna nafasi kwa wazazi /walezi wawili tu kuwepo, Watoto na vijana, kaka na dada hawaruhusiwi kuingia.

Kula na kunywa humo ni marufuku kwa wote, watoto na wazazi, ili wanaofunga wasijisikie vibaya.

Unashauriwa kuacha nguo nzito, koti na mabegi, kwenye wadi ama katika kabati maalum yenye ufunguo inayopatikana katika chumba cha kusubiri, (waiting area)

Simu za mkononi sharti zifungwe. Sababu: zinaweza kudhuru vifaa mbalimbali zinazotumia umeme, tena zinasumbua sana wanaoamka baada ya usungizi/narcosis.

Watoto wapo wanaohitaji kubembelezwa na kufarijika, ambapo wengine wengi zaidi , wanauzingizi mzito na wanahitaji kujiamsha wenyewe pole pole.

Watoto wote wanapata hewa zaidi, oxygene, inayopulizwa kwenye sura, (mdomo na pua)

Wanaangaliwa kila wakati vile wanayopumu, mapigo ya moyo na hali ya damu kushiba oxygene.

Jinsi watoto wanaojisikia katika kupata narcosis ina tufauti sana. wakati wote, muda wa usingizi na baadaye, kuna uangalifu sana kuzuia na kupunguza shida yo yote inayoweza kutokea. Ingawa jitihada hiyo kuna shida inayoweza kutokea, k.m.

  • Kuchoka na kusikia kizunguzungu
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Kuumwa kooni
  • Kikohozi
  • Kuwashwa kwenye mshipa wa damu, pale pale sindano, bomba imeingizwa.
  • Usumbufu kutoka bomba ya kuondoa majimaji kwenye kidonda (drainage) ama kutoka bomba kwa mrija wa mkojo (urine catheter)

Mtoto akiishapasuliwa anapata dawa ya kupunguza maumivu kila akihitaji mpaka maumivu yamepungua kabisa. Baada ya upasuaji maalum, dawa ya kupunguza maumivu yanatolewa kwa bomba na sindano, mfano ya dripu.Wauguzi wanaangalia mtoto mara kwa mara kwa kuhakikisha asiwe na maumivu au shida yo yote.

Wewe kama mzazi/jamaa ni vizuri kuwaambia wauguzi ukiona mtoto anasikia maumivu.

Waganga wakiishaona kwamba hali ya mtoto inaridhisha atarudi kwenye wadi alipotoka.

//Search

twitter icon

Astrid Lindgren ChildrenĀ“s Hospital |Ā Karolinska University Hospital 171 76 Stockholm


© Karolinska University Hospital

mail
Logotype