Mandalizi kabla ya Narcosis


Atakapotiliwa usingizi habari ya afya yake mtoto ni muhimu sana. Ni kwa hiyo wafanyakazi watauliza maswali mengi kidogo.

Kwa wote:

  • Magonjwa yote aliyokuwa nao na mpaka sasa ?
  • Allergi, reaction. Kutokupatana kiafya na vitu maalum ?
  • Dawa anayotumia sasa na kwa muda wa mwezi mmoja nyuma ?
  • Kama amewahi kupata narcosis na ikiwa ilimwletea shida yo yote.?
  • Kama jamaa ya karibu wamepata shida yo yote katika kupata narcosis ?
  • Uzito wake ?
  • Meno , kuna jino linalolegea ?
  • Shida ya kusikia kichefuchefu na kutapika katika kusafiri kwa gari n k ?

Maswali zaidi kwa vijana:

  • Matumizi ya tumbako ?
  • Habari ya mimba ?

Ujitahidi pia kuambia mtafu kama mtoto anayo au amewahi karibuni kuwa nayo shida yo yote ya koo na matezi ya kooni neumonia, bronchitis, kifaduru n.k. Kumbuka kutaja kama mtoto amekuwa na mafua/makamasi karibuni.

Dalili za majonjwa ya koo , k.m. homa, kikohozi, shida ya kupumua sawasawa, kuziba kwa pua, au makamasi kutiririka.Hali kama hizo zinapunguza usalama kwa atakayetiliwa usingizi kwa narcosis, na huenda upasuaji/surgery, itaahirishwa kwa muda.

Kumbuka pia kutaja kama mtoto amewahi kupata kichefuchefu na kutapika akisafiri kwa gari.

//Search

twitter icon

Astrid Lindgren ChildrenĀ“s Hospital |Ā Karolinska University Hospital 171 76 Stockholm


© Karolinska University Hospital

mail
Logotype