Wadi wa Upasuaji


Mtoto aingiamo anaweza kusindikizwa na mzazi/mlezi mmoja tu.

Anayesindikiza anapata nguo maalum kwa kutunza usafi wadini, kanzu, kofia ya plastiki na viatu.

Baadaye mtoto analazwa kwenye meza fulani na kuingizwa kwenye chumba cha upasuaji. Mtoto akiandaliwa kwa narcosis,( usingizi na ganzi), yafaa mzazi/mlezi akae karibu naye.

Dawa ikiingizwa kwa sindano ndani ya mshipa wa damu, atapata usingizi mzito moja kwa moja. Akiishasinzia, msindikizaji pamoja na baadhi ya staff wataondoka kwenda kukaa katika chumba kingine cha karibu ambapo watasubiri.

Wasazi wengi wanajisikia vibaya wakiona jinsi mtoto anavyopata usingizi haraka na wanachukia kumwacha mtoto mikononi ya wageni. Hapo yafaa kukumbuka kuwa mtoto kwa muda wote wa usingizi huo anaangaliwa kwa makini na wataalamu na vifaa vyao vya sayanzi.

//Search

twitter icon

Astrid Lindgren ChildrenĀ“s Hospital |Ā Karolinska University Hospital 171 76 Stockholm


© Karolinska University Hospital

mail
Logotype