Nitamwelezaje mtoto wangu?


Jinsi anavyofahamu mwili wake, na kuwaza juu ya mwili , sehemu za mwili na magonjwa, inatofautiana kwa kutegemea fahamu yake na umri wake.

Hata hofu yahusu magonjwa na maumivu inategemea kukomaa kwake na inakwenda sambamba na vitisho vingine katika umri tofauti.

Jinsi mtoto anavyojisikia akiugua, inategemea pia alivyowahi kukutana nayo yahusu kuugua na kutibiwa. Alivyoona nyumbani,maoni na matumaini yao wazazi. Utamaduni tofauti unaleta mawazo tofauti.

Mtoto akiisha kujiandaa kabla ya matibabu hospitalini, atajisikia vizuri zaidi kuliko mtoto anayekosa kufahamu hata kidogo. Kwa kumweleza vizuri na mapema, hofu na huzuni hupunguzwa. Atatulia na kuwa na moyo thabiti.

Hitaji ya maelezo na ujuzi hutegemea umri wake.Wakati wote ufafanuzi utakuwa wazi na ya kweli, kwa lugha inayofaa kwa umri na maendelo yake mtoto.

Ni ya maana pia kumweleza kwa ufupi na urefu unaofaa na kwa wakati wake.

Shika nafasi ambapo mtoto amepumzika, anapotulia na pia anapokuwa na maswali.

Uwe tayari kumsikia.Angalia dalili na kuzitafsiri. Jaribu kugundua anavyojisikia.

Mtoto aliyewahi kutibiwa hospitalini haepuki hofu na mashaka. Hata kidogo. Anaweza kukumbuka mambo fulani yaliyomtisha, na anajua yatakayofuata. Kwa hiyo ni muhimu kumweleza tena kama mara ya kwanza.

Mtoto, kwake ni vigumu kufahamu na kuhisi itakayotokea na atakavyojisikia katika shida na mkazo mbeleni. Kwa kumsaidia kupambana na mambo hayo, kaa naye kwa kusemezana juu ya hali tofauti ambazo huenda atakayokuta ,na atakavyoweza kujisika.

Mwambie kama ni halali kabisa kuonyesha wazi anavyojisikia.

Mkumbushe pia, kwamba ”kuuliza si ujinga” hata kidogo!

Wewe mzazi ukishindwa kumjibu , pendekeza aandike au achore maswali yake na kuleta hospitalini.

Ni muhimu kumweleza mtoto na ni muhumu pia kufahamu wakati upi unaofaa. Watoto wadogo inafaa kuwaeleza ikibaki muda mfupi tu kabla ya kutibiwa. Hawaelewi maelezo kwa urefu, pia watasahau haraka.

Wewe unayemfahamu mtoto utaweza kumsaidia kwa kufafanua kwa lugha inayofaa zaidi. Kila mtoto ni tofauti na mwingine

Watoto wadogo miaka 0 –3

Kwa mtoto mchanga atakayepata narcosis, bila shaka ni wewe mzazi unayesikia usumbufu na kutaabika zaidi kuliko mtoto wako. Hii ni kawaida, lakini ujue kwamba mtoto mchanga kabisa ,umri wa miezi 0 – 2 kwa kawaida atasikia amani kwa ye yote ambaye atamwuguza vizuri.

Baadaye watazoea mapema na kujisikia vizuri pamoja na wa nyumbani, hapa hapa watatulia na kuwa na amani. Kwa umri wa miezi nane hadi miaka miwili , watoto kwa kawaida wanaonyesha hofu kwa wageni. Ni wewe mzazi unayeweza kumtuliza ukiwa karibu naye.

Kwa mtoto wa umri huu itatosha kabisa kumfariji na kumweleza kwa neno fupi tu itakavyotokea Usijaribu kumpasha habari ya hali yake au atakavyotendewa, hawezi kuifahamu .Huenda utaweza kumwambia kwamba mwanasesere wake anaumwa, na mtahitaji kwenda pamoja hospitalini.Onyesha ni wapi anapoumwa mwanasesere, na baadaye kwamba mtoto pia atapimwa jinsi hiyo hiyo.

Mtoto ambaye hajafikisha umri wa miaka mitatu, hana habari ya muda, masaa na masiku, kwa hiyo, usianze kueleza mapema, ila siku moja kabla au siku ile ile.

Watoto wa chekechea na shule wa awali, wa miaka 3 –6

Watoto hawa wanawaza mengi juu ya mambo ya ajabu. Hawajapata kufahamu mambo ya uhakika .Wanaunda ”ulimwengu wao”, kabla ya kupata ufahamu wa vitu vilivyo na mambo yalivyo.

Wanaoona na kusikia, yote wanaopata kwa milango ya fahamu ,wanaunganisha na “kuunda ukweli wao”. Wanavyofahamu ulimwengu hutegemea akili kukomaa.

Pengine hawana habari ya ipi inayotangulia, mwanzo na matokeo. (cause and effect)

Hayo yanaweza kusababisha kwamba wafahamu magonjwa kwa jinsi iisivyo kabisa.

Tena hawawezi kutofautisha kati mambo ya ndani na mambo ya nje. Wakisikia maumivu wanaweza kuitafsiri vingine, yaani maumivu imesababishwa na mambo mengine.

Katika mchezo huu, habari za mwanasesere mgonjwa itamwelimisha mtoto na kumwandaa kwa mambo atakayoyakuta mbeleni hospitalini.

Kwa hiyo, utapata msaada kubwa kwa kutumia mwanasesere na mchezo “mkoba wa daktari”

Watoto wa umri wa miaka 6 – 12

Watoto wanaanza kufahamu tofauti ya kuwaza, yaani kuunda moyoni, kuota akiwa macho, na jambo la uhakika.Wanajua za mwili, kama kiwiliwili, mikono, miguu na viungu vya ndani/matumbo.

Wanafahamu tofauti ya ujenzi, muundo ya kiungu, na kazi ya viungu mbalimbali

Sasa mtoto anafahamu kwamba mtu anaweza kuumwa kwa ajili ya magonjwa na madhara ya kiungu cha ndani, na si kwa mapigo na majeraha tu.

Wanafahamu: Magonjwa si tokeo la ajabu-ajabu. Magonjwa si kulogwa au adhabu kwa makosa yake anayeumwa. Magonjwa yana weza kusababishwa na chembe ndogo ndogo kama virusi na bakteria.

Lakini hata mtoto mkubwa pengine anaweza kuwaza kama mtoto mdogo, kuwaza ”kiuganga”, hasa akipata taabu.

Wa umri huu wanajali mwili zaidi.Pengine wanahisi kwamba sehehemu ya mwili itakatwa na kuharibika.

Kwa hiyo ni muhimu kueleza waziwazi utaratibu utakaofuatwa na sehemu gani zitakazotibiwa. Hakikisha ajue kama si sehemu zote zitokaoguswa.

Watoto katika umri huu huenda wanagopa sana vifaa na mitambo vya saiansi ya kihospitali

(technical equipment)

Katika umri huu wanaanza kuwaza juu ya mauti na kuogopa kufa. Kifu na kulala usingizi yaafanana, na wengi wanaogopa kwamba hawataamka tena baada ya kupasuliwa.

Watoto hawa wanaweza kuzungumza na kutuambia wanavyojisikia.Wanafahamu sababu ya kupimwa na wanajali matokeo ya vipimo. Kuliko watoto wadogo ni wadadisi, wanataka kujua. Jaribu kusimulia na kueleza kufuatana na maswali yake.

Inafaa kumweleza mtoto kama wiki moja kabla ya kwenda hospitalini kwa matibabu.

Vijana, 13 –18

Muda huu ni ya maana sana katika maisha. Kuna mabadiliko makubwa kimwili na kinafsi, Hofu kutokuwa sawa na binadamu wengine, hofu kwa ajili ya mwili kutokubadilika zambamba na vijana wenzake, ama kujiangalia na kujuta juu ya sura au mwili.Mara nyingi wanajiangalia na kuona kuwa wote wengine ni wazuri zaidi.

Katika muda huu ya kubalehe mwili ni muhimu sana sana. Kwa hiyo, kutibiwa kwa njia ya upasuaji, au kulazwa na kuuguzwa na wageni wanaoona uuchi wao, ni pigo linaloweza kuvunja moyo.

Vijana wanajishugulikia wenyewe sana na inaonekana kama ubinafsi ambapo wanajijali wenyewe kuliko wote wengine. Hawana habari ya kuwa hata wengine wanaowasidi kwa umri wamekabiliwa na shida hiyo , kubalehe.

Vijana wanahitaji kujitenga na wazazi na kuonyesha kwamba wamekomaa.Wanahitaji kujitegemea kwa namna fulani.

Vijana hawataki kabisa kuongea na wazazi juu ya maisha, au kushauriwa.

Kuugua ni kama kurudi nyuma tena na hii inawasumbua sana. Kwa sasa wanaonekana wakubwa, wanahitaji kuangaliwa kama watu waliokomaa, lakini ndani kabisa, bado anakuwa mtoto mwenye mashaka na huzuni juu ya ugonjwa .Ujue mzazi, huyu bado anakuhitaji na anataka kuwa karibu nawe. Hawezi kuikiri kwa maneno, lakini usiwe mbali naye. Anahitaji msaada wako na kushauriwa nawe.

Atakapopata narcosis,huenda anahofia kwamba ataamka katika kupasuliwa na kuumia sana. Huenda anaogopa vilevile kutokuamka, kulala kabisa. Tena wanaogopa kuchanganyikiwa, kusemasema au kushindwa kujitawala kwa haja kubwa na ndogo.

Kijana anapenda kutendewa na kuangaliwa karibu sawa na mtu mzima, lakini si mia kwa mia.

Anahitaji kufahamishwa karibu kila neno. wameishajua habari za mwili, saiyansi yahusu mwili wa binadamu, viungu vya nje na vya ndani , jinsi vinavyofanya kazi.

Anaweza pia kufikiri na kufahamu mambo yanayoweza kutokea. Kwa hiyo, anahitaji kuelezwa kwa urefu juu ya yote alivyopanga daktari. Aelezwe sababu ya vipimo mbalimbali na kuwa matokeo ya vipimo vitasababisha matibabu maalum. Umsaidie katika kuuliza, kusikia na kufahamu.

Ili apate muda wa kusoma, kuuliza . kufikiri, kujiandaa, anza mapema kumtayarisha.

Umtie moyo kuandika maswali juu ya mambo yanayosumbua. Kuuliza si ujinga na akielezwa vizuri na watalaamu moyo wake unaweza kutulia.

Referenses

Bishofberger, E., Dahlquist, G., Edwinsson-Månsson, M., Tingberg, B. & Ygge, B. (2004). Barnet i vården. Stockholm: Liber.

Jylli, L., Olsson, G. (2005). Smärta hos barn och ungdomar. Lund: Studentlitteratur.

Tamm, M. (2004) Barn och rädsla. Lund: Studentlitteratur.

//Search

twitter icon

Astrid Lindgren Children´s Hospital | Karolinska University Hospital 171 76 Stockholm


© Karolinska University Hospital

mail
Logotype