Kufunga, kujinyima chakula na kinywaji


Kwa usalama wa afya ya mtoto ni muhimu sana kufuata maagizo inayotolewa hospitalini. Sababu ni hatari ya kutapika uzingizini. Matapisha yanaleta hatari kubwa katika njia za pumzi.

Kwa habari ya kufunga kabla ya narcosis, wanatofautisha kati ya vyakula mbalimbali jinsi vinayotumia muda kuyeyuka katika mfuko wa tumboni. Vinywaji , vitu vya hali majimaji vinapita mfuko wa tumbo haraka zaidi kuliko chakula kigumu.

Vya majimaji vinatumia muda mfupi zaidi kuliko vyakula vigumu. Lakini ujue kama vinywaji ya aina mbali mbali havilingani. Juice ya machungwa, maziwa yaliyoganda na soda k.m. zinachukua muda mrefu zaidi kuliko maji ya kawaida, Juice ya tofaa/applejuice, na kahawa bila maziwa (black coffee)

Maziwa ya mama na mifano yake ni kitu cha katikati ya kiywaji na chakula. Kama kuna mashaka yo yote katika maagizo uliyotolewa kwa mtoto wako, tafadhali uliza katika wadi husika hospitalini.

//Search

twitter icon

Astrid Lindgren ChildrenĀ“s Hospital |Ā Karolinska University Hospital 171 76 Stockholm


© Karolinska University Hospital

mail
Logotype