Aina ya narcosis na kutiliwa ganzi (Narcosis na anesthesia)


Neno narcosis maana yake ni sawa ya anesthesia ”kutokusikia kuguzwa ” ”Kupata ganzi”

Katika upasuaji au kwa kupimwa, kuna njia nyingi ya tia narcosis na anesthesia.

Inayochaguliwa inatofautiana kwa kuangalia umri wake mtoto , aina ya upasuaji (surgery) na hali yake kiafya.

Anayeamua ni aina gani inayofaa zaidi, ni daktari bingwa (fani ya narcosis) baada ya kumpima mtoto na kusungumza na wazazi.

Narcosis ya kutiliwa usingizi (general anesthesia)

Aina hii inatumika zaidi. Mtoto anasinzia kabisa na hasikii maumivu yo yote.

Dawa inaingizwa katika mshipa kwa sindano, au kwa njia ya kuvuta pumzi pamoja na dawa., kutoka bomba fulani inayowekwa karibu na pua na mdomo.

Wataongeza dawa kwa njia hizo ili asinzie muda unaotakiwa, pamoja na dawa ya kutuliza maumivu.

Ganzi kwa sehemu fulani (regional anesthesia)

Ni dawa ya ganzi inayoingizwa kwa sindano katika sehemu fulani yenye neva nyingi. Hii inatia ganzi kabisa hasa kwa sehemu ya mwili inayohusika na neva hiyo. Kawaida sindano hii ya ganzi, anapata mtoto akiisha kusinzia.

Kwa mtoto aina hii ya ganzi inatumika hasa pamoja na ”general anesthesia” (hapo juu) ili kuongeza ganzi kwa sehemu fulani ikitakiwa kwa kuzuia maumivu kabisa.

Aina moja ya anesthetics hiyo ni : ”ganzi kwa njia ya uti wa mgongo”

Ganzi kwa sehemu ndogo (lokal anesthesisa)

Ni kupakwa dawa yenye ganzi au ganzi kuingizwa chini ya ngozi kwa sindano.

Kwa njia hizo mbili, maumivu yatazuiliwa. Aina moja ni EMLA, dawa inayopakwa pale pale atakapopata sindano.

Local anesthesia inatumika pia pamoja na general anesthesia kwa kuzuia maumivu wakati wa kupasuliwa na baada ya kuamka.

//Search

twitter icon

Astrid Lindgren Children´s Hospital | Karolinska University Hospital 171 76 Stockholm


© Karolinska University Hospital

mail
Logotype